Yesu Ajapo kwa ajili yako
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 4
SOMO 08Hatua 1 ya 4 (25%)

Yesu Ajapo kwa ajili yako

Baada ya miaka mingi ya kutendewa vibaya, Armando Balladares alikuwa amekonda vibaya sana na kulemaa akiwa kama kinyago tu cha vile alivyokuwa mara ya kwanza. Alikuwa amevutiwa sana na imani yake iliyomletea mateso. Muda mfupi baada ya watu wale wawili kuoana katika sherehe ya kuwafungisha ndoa yao iliyoendeshwa kiserikali katika uwanja wa gereza lile, Martha alilazimka kuhamia Miami.

Kutengana kwao kulileta uchungu mwingi sana. Lakini Armando alifanikiwa kutuma kwa siri ahadi yake kwenda kwa mpenzi wake. Juu ya kipande cha karatasi kilichotupwa aliiandika ahadi yake hii:

"Nitakuja kwako. Singe hizo zilizo katika upeo wa mgongo wangu hazitakuwa na maana tena."

Mfungwa huyo alidhamiria kwamba kwa njia fulani yeye na Martha wangetoa ahadi zao ndani ya kanisa mbele za Mungu. Siku moja muungano wao ungekamilika. " Wewe u pamoja nami daima" alimwambia mwanamke yule.

Ahadi aliyotoa Armando ilimfanya aendelee kuishi katika miaka aliyotendewa vibaya sana ambayo ingekuwa imeivunja mioyo ya wanaume wengi. Nayo ilimfanya Martha aendelee kuishi. Alifanya kazi bila kuchoka ili kuyaamsha mawazo ya umma yapate kutambua hali mbaya iliyomkabili mumewe. Yeye hakukata tamaa kamwe.

1. Ahadi

Kuna nyakati fulani sisi tunaweza kujaribiwa na kushangaa, je! hivi kweli siku moja Kristo atashuka na kuja tena katika mbingu hizo za samawi zilizo juu yetu kwa muungano ule wa ajabu pamoja nasi? Mwisho huo wenye furaha wa historia hii ndefu, yenye misiba mingi ya ulimwengu, unaweza kuonekana kama ni mzuri mno kiasi cha kufikiriwa kuwa si wa kweli kwetu sisi. Lakini kuna kitu kimoja ambacho kinaweza kulifanya tumaini letu kuwa hai mioyoni mwetu. Na kitu hicho ni ahadi ya Yesu pekee aliyoitoa kwamba yeye atakuja tena. Muda mfupi tu kabla hajajitenga mbali na wanafunzi wake, Yesu alitoa ahadi hii:

Yohana 14:1-3
"Yesu aliwaambia, Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu; niaminini na mimi pia. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama isingekuwa hivyo, ningekwisha waambieni. Sasa nakwenda kuwatayarishieni nafasi. Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi, nitarudi na kuwachukueni kwangu, ili nanyi mwe pale nilipo mimi"

Kabla Yesu hajapaa kwenda mbinguni, aliwaahidi wafuasi wake, akisema "NITAKUJA TENA!" Aliahidi kurudi tena kuja kuwachukua wale wote wanaomtegemea ili awape mahali maalum alipowaandalia. Maandiko yanasema juu ya kuja kwake mara ya pili karibu mara 2,500 hivi. Ukweli kwamba Kristo anakuja mara ya pili katika ulimwengu huu ni wa hakika kama ulivyo uhakika kwamba yeye aliwahi kuishi hapa dunaini miaka elfu mbili iliyopita.

Zamani sana Mungu aliahidi kwamba Masihi angekuja, yaani Mkombozi ambaye angechukua mwilini mwake uovu wetu na kutoa msamaha wake kwa ajili ya dhambi za wanadamu. Ahadi ile ilionekana kana kwamba ilikuwa ni nzuri mno kiasi kwamba isingeweza kuwa ya kweli kwa wengi katika ulimwengu ule wa zamani ambao walikuwa wakiendelea kufanya kazi zao kwa bidii katika maisha yao yote. Lakini kweli Yesu alikuja na kufa juu ya msalaba. Ahadi ilitimia kweli kwa utukufu kuliko vile watu walivyowaza kwamba uwezekano kama ule ungekuwapo. Ahadi yake ya kurudi tena pia itakuwa ni ya kweli. Sisi twaweza kumtegemea yeye atupendaye, kurudi tena na kuwakusanya wale ambao kwa ajili yao amelipa gharama kubwa mno isiyokadirika.

Katika kipindi chote cha kufungwa kwake, Armando aliendelea kutuma kwa Martha kwa siri mashairi, ujumbe, na picha alizochora. Naye [Martha] alifanikiwa kuyachapisha baadhi ya maandiko yale. Ufasaha wake [yale maandiko] uliyavuta mawazo ya ulimwengu. Serikali zikaanza kumbana Castro ili awaachilie wafungwa wale waliofungwa kwa sababu ya kuzifuata dhamiri zao. Rais wa Ufaransa akaingilia kati na hatimaye katika mwezi wa Oktoba mwaka wa 1982 Armando alipakiwa katika ndege iliyokuwa ikienda Paris. Ilikuwa ni vigumu sana kwake kuamini kwamba alikuwa huru-hata wakati ndege ile ilipotua. Lakini basi, baada ya miongo miwili [miaka ishirini] ya mateso na shauku yake ya kungoja, Armando alikimbia na kukumbatiwa na mikono ya Martha.

Miezi michache baadaye katika kanisa la Miami la Mtakatifu Kierani wale wawili wakasimama na kurudia kutoa kiapo chao cha ndoa. Hatimaye muungano wao ukawa umekamilika. Ahadi ikawa imetimizwa: "Nitakuja kwako."

Je, waweza kufikiria ni muungano wa ajabu jinsi gani utakaokuwako hatimaye tutakapoweza kumwona Kristo uso kwa uso? Kuja kwake katika utukufu wake kutazimeza huzuni zetu zote pamoja na kuvunjika mioyo kwetu kote, kutayafutilia mbali maumivu yetu yote tuliyoyaficha mioyoni mwetu. Kurudi tena kwa Yesu kutakidhi shauku zetu zenye kina sana na matarajio yetu ya kusisimua sana. Kisha tutaingia katika umilele wa muungano wa karibu sana na mtu yule wa ajabu sana katika Malimwengu yote. Yesu yu aja upesi! Je, wewe unayo shauku ya kukutana naye?