Sehemu 1
Siku moja Jimi alimwuliza mtu mmoja anayekana kuwa kuna Mungu endapo alipata kujaribu sana, hata kwa dakika chache tu, kupigana na wazo lisemalo kwamba huenda Mungu yuko."
Sawa kabisa!" mkana Mungu yule akajibu, akimwacha Jimi na mshangao. "Miaka mingi iliyopita, mimi nilikuwa karibu sana nigeuke na kuwa mtu anayemwamini Mungu. Nilipokiangalia kile kiumbe kidogo sana - lakini - kikamilifu katika kitanda chake kidogo, nilipochungulia na kuviona vidole vile vidogo fahamu za kwanza za kutambua, nilipita katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo katika hiyo mimi nilikuwa karibu kabisa niache kuwa mkana Mungu. Kule kumwangalia mtoto yule kulikuwa kumenishawishi karibu kabisa kuwa hapana budi Mungu alikuwa yuko."
