Siri ya pumziko la Mbinguni
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 6
SOMO 16Hatua 1 ya 6 (17%)

Siri ya pumziko la Mbinguni

Miaka michache tu iliyopita wengine walikuwa wakibashiri kwamba muda si mrefu tungekuwa na muda mwingi sana wa mapumziko ambao tungeshindwa kujua tufanye nini nao. Hizi zilikuwa ndizo sababu nzuri kwa ubashiri ule wenye matumaini. Katika miji mikuu ya ulimwengu makompyuta yalikuwa yakizisaga-saga kazi ambazo zingechukua mwezi mzima kuzifanya kwa sehemu tu ya nukta moja. Na yale maroboti yalikuwa yameanza kuzifanya kazi ngumu sana za kuchosha katika viwanda vya kutengeneza mashine nzito.

Lakini baada ya makompyuta hayo kutoa mfumo wao na maroboti kufanya kazi zao, bado tunakosa hata pumzi kuzifanya kazi hizo muda wa siku hizi. Zaidi ya yote, familia zinakosa muda wa kukaa pamoja. Waume na wake zao huona vigumu kupanga "muda unaofaa" wa kuwa pamoja na watoto wao, licha ya wao wenyewe kuwa na muda mchache wa kuwa pamoja.

Utafiti mmoja uliofanywa katika jumuia moja ndogo ulionyesha kwamba wastani wa muda kila siku ambao mababa wanatumia wakiwa peke yao na watoto wao wadogo sana ulikuwa nukta 37! Familia hazina muda, wala hazina mawasiliano.

Je! Tunawezaje kupunguza hiyo kasi tuliyonayo kwa kiasi cha kutosha kuweza kuwa na uhusiano wetu tena?

1. Dawa Ya Maisha Yaliyojaa Mahangaiko

Yesu anayajua matatizo ya familia zilizo chini ya shinikizo hilo, naye anataka sisi tujue kwamba pumiziko la kiroho ni sehemu ya maisha bora; 

Mathayo 11:28, 29.
"NJONI KWANGU, ninyi nyote mliochoka na maisha na kulemewa na mizigo, NITAWAPUMZISHA… MJIFUNZE KWANGU, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata RAHA NAFSINI MWENU."

Biblia inatushauri kuionja hiyo raha kwa njia mbili: Kumwendea Kristo kwa kutegemea msingi huu wa aina mbili, KILA SIKU na KILA JUMA.