Siri ya furaha
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 5
SOMO 15Hatua 1 ya 5 (20%)

Siri ya furaha

Mwaka 1943, majeshi ya Uvamizi ya Kijapani yaliwaamuru wale "Wananchi Maadui" wa Kimarekani na Ulaya kwenda katika kambi la waliotekwa vitani katika lile Jimbo la china la Shantung.

Walilazimika kustahimili miezi mingi ya kuchosha sana, ya kukata tamaa, ya kusongamana pamoja na ya hofu. Watu wenye tabia tofauti waligongana, hasira zililipuka. Magomvi madogo madogo yaliongezeka sana.

Lakini mtu mmoja alielezwa na mfungwa mmoja wa kivita kwamba "bila shaka lolote alikuwa ni mtu aliyehitajika sana na kuheshimiwa sana, tena aliyependwa sana katika kambi lile. "-Eric Liddell, Mmishonari kutoka katika nchi ya Waskoti (Scotland).

Malaya mmoja wa Kirusi katika kambi lile baadaye aliweza kukumbuka ya kwamba yule Liddell ni mwanaume peke yake aliyeweza kumtendea yule mwanamke jambo lolote bila kutaka kulipwa kimwili. Mwanamke yule alipokuja mle kambini kwa mara yake ya kwanza, akiwa peke yake, na mwenye kudharauliwa, ndiye aliyemtengenezea yeye baadhi ya rafu za kuwekea vitu vyake.

Mfungwa wa vita mwingine alikumbuka kwamba, "yeye alikuwa na mbinu ya upole, na ya kuchekesha iliyozilainisha hasira zao zilizovurugika vibaya".

Katika mkutano mmoja uliojaa hasira wa wafungwa wale wa kivita, kila mmoja alikuwa akitoa madai yake kwamba mtu fulani mwingine ndiye angefanya kitu fulani kwa wale vijana watukutu wenye umri wa kuanzia miaka kumi na mitatu hadi kumi na tisa (matineja) ambao walikuwa wanajitia katika matatizo. Liddell akatoa suluhisho lake. Aliandaa michezo ya kujiburudisha, ufundi wa kutengeneza vitu kwa mikono, na madarasa kwa ajili ya watoto wale, na kuanza kutumia wakati wake wa jioni pamoja nao.

Liddell alijipatia sifa na utukufu katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 192, alijinyakulia nishani ya dhahabu katika mbio za mita 400. Lakini katika uwanja ule mdogo sana wa kambi lile alijionyesha pia ya kuwa ni mshindi katika zile mbio za Kikristo, akajipatia sifa kutoka kwa wafungwa wa vita wale walioipenda sana dunia hii.

Je! Ni kitu gani kilichomfanya kuwa mtu wa aina yake? Ungeweza kuwa umeigundua siri yake saa 12 kila asubuhi. Ule ndio wakati alipotoka kimya kimya kwa kunyatia akiwapita wenzake waliolala usingizi, na kutulia kimya mezani, na kuiwasha taa ndogo ili itoe mwanga wa kumwezesha kuliona daftari lake ndogo na Biblia yake. Eric Liddell alitafuta neema na nguvu kila siku kutoka katika utajiri wa Neno la Mungu.

1. Kitabu Cha Mwongozo Wa Kuishi Mtindo Wa Maisha Ya Kikristo

Biblia iliandikwa kama kitabu cha Mwongozo kwa Mkristo. Kimejaa visa vingi vya watu halisi walio kama sisi waliokabiliwa na changamoto zile zile tunazokutana nazo kila siku. Kuwafahamu wahusika hao wa Biblia - furaha na huzuni zao, matatizo yao na nafasi zao nzuri walizopata hutusaidia sisi kukomaa kama Wakristo.

Mtunga Zaburi, Daudi aonyesha mfano wa kulitegemea Neno la Mungu kila siku kwa kulilinganisha na mwanga wa tochi (kurunzi);

Zaburi 119:105
"Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu."

Nuru tunayoipata kila siku kutoka katika Biblia inafunua wazi sifa zile tunazozihitaji katika maisha yetu na kanuni za kukua kiroho. Zaidi ya hayo yote, Biblia inatuonyesha Yesu, Nuru ya Ulimwengu. Maisha yetu yana maana tu anapoyaangazia Yesu kwa Nuru yake.

2. Urafiki Unaotubadilisha Kabisa

Kristo anataka Biblia kwako iwe kama barua uliyoandikiwa mwenyewe itokayo kwa rafiki yako wa karibu sana.

Yohana 15:15.
"Ninyi nimewaita rafiki, kwa sababu kila kitu nilichokisikia kwa Baba nimewajulisheni."

Yesu anatutakia mema matupu. Neno lake linatuingiza sisi katika familia ile ya ndani ya Mungu; Yaani, ya wale anaowaambia siri zake na kuwafundisha yeye mwenyewe.

Yohana 16:33.
"Nimewaambieni ninyi mambo hayo, ili ndani yangu ninyi mweze kuwa na amani."

Ili kuweza kuionja amani hiyo, na uhusiano huo thabiti pamoja na Kristo, ni lazima tuzisome barua zake anazotutumia. Hivyo ndivyo Biblia ilivyo: ni barua zitokazo mbinguni. Usiziache barua hizo bila kuzifungua. Ujumbe uwezao kuyabadilisha kabisa maisha yako ambao unauhitaji umo ndani ya Neno hilo.

Hapa upo ushuhuda mmoja kamili uhusuo matokeo ya kuisoma Biblia. "Mimi nilihitaji msaada, nao niliupata ndani ya Yesu. Kila haja yangu ilitimizwa, njaa ya nafsi yangu ilishibishwa; kwangu Biblia ni ufunuo wake Kristo. Namwamini Yesu kwa sababu yeye kwangu ni Mwokozi wa Kimbingu. Naiamini Biblia kwa sababu nimeiona kuwa ni sauti ya Mungu rohoni mwangu. " - The Ministry of Healing, uk. 461.

3. Miongozo Ya Kuishi Kwa Kufuata Biblia Na Zile Amri Kumi

Kuziangalia kwa kifupi tu hizo Amri Kumi kutatusaidia kuelewa kwa nini hizo pamoja na Biblia hujenga msingi muhimu sana wa maisha yaliyo manyofu.

Amri hizo kwa kawaida huangukia katika sehemu kuu mbili. Zile nne za kwanza hufafanua uhusiano wetu na Mungu, na zile sita za mwisho hufafanua uhusiano wetu na watu wengine. Zinapatikana katika Kutoka 20:3-17.

Amri mbili za kwanza zinaelezea uhusiano wetu na Mungu pamoja na ibada yake.

I. "Usiwe na Miungu mingine ila Mimi".

II. "Usijifanyie sanamu ya kuchonga. Usizisujudie wala kuzitumikia…"

Amri ile ya 3 na ya 4 hueleza kwa juu juu tu uhusiano wetu na jina la Mungu na siku yake takatifu.

III. "Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako…"

IV. "Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako…"

Amri ya 5 na ya 7 inaimarisha vifungo vya familia.

V. "Waheshimu baba yako na mama yako…."

VI. "Usizini."

Amri ya 6, 8, 9 na 10 hutulinda sisi katika uhusiano wetu kijamii.

VII. Usiue."

VIII. "Usiibe."

IX. "Usimshuhudie jirani yako uongo."

X. "Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako….. wala chochote alicho nacho jirani yako."

Amri hizo kumi zinaweka mipaka ya uhusiano wetu kwa Mungu na kwa watu wengine. Hizo ni nguzo za kutuongoza katika mtindo wa maisha yetu ya Kikristo.