Makao yako ya Mbinguni
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 4
SOMO 09Hatua 1 ya 4 (25%)

Makao yako ya Mbinguni

Marko Polo aliporudi kwenye mji kusafiri miaka mingi katika nchi za mashariki, rafiki zake walidhani kwamba safari zake zile ndefu sana zilikuwa zimemfanya kuwa mwehu. Alikuwa na hadithi nyingi za kusimulia zilizokuwa hazisadikiki.

Marko alikuwa amesafiri hadi kwenye mji uliojaa fedha na dhahabu. Alikuwa ameyaona mawe meusi yaliyokuwa yakiungua moto, lakini hakuna hata mmoja wao aliyekuwa amepata kuzisikia habari za makaa ya mawe. Aliiona nguo iliyokataa kuwaka moto hata kama ilitupwa katika ndimi za moto, lakini hakuna hata mmoja wao aliyekuwa amepata habari za asbestos. Aliongea juu ya nyoka wakubwa urefu wao hatua kumi na mataya yao mapana ya kutosha kumeza mtu mzima, kokwa ambazo ukubwa wake ulikuwa kama kichwa cha mtu na nyeupe kama maziwa ndani yake [nazi], na kitu fulani kilichokuwa kikibubujika kutoka ardhini ambacho kilizifanya taa ziwake kabisa. Lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa amepata kuona, mamba, nazi, wala yale mafuta yasiyosafishwa. Walicheka tu kusikia visa kama vile. Miaka mingi baadaye, Marko alipolala kitandani pake akiwa anakufa, mcha Mungu mmoja aliyekuwa kando ya kitanda chake akamsihi kuzikana zile hadithi zake ngumu za kusadadikika alizokuwa amezisimulia. Lakini Marko alikataa, alisema: "Zote ni za kweli kwa kila kipengele. Kusema kweli, mimi sijasimulia nusu ya yale niliyoyaona."

Waandishi wa Biblia watuonyeshao sisi picha kidogo tu ya mbinguni ambazo huonekana kana kwamba zinatoa mwangwi wa hisia aliyokuwa nayo Marko Polo. Katika maono yao walipatazama mahali pale palipokuwa paking'aa mno, pa ajabu mno, hata waliweza kueleza sehemu ndogo tu ya yale waliyoyaona. Nasi tunakabiliwa na changamoto ifananayo na ile ya marafiki wa Marko Polo. Hatuna budi kujaribu kuwaza habari za "mamba na nazi," yaani, mambo ambayo sisi hatujapata kamwe kuyaona kwa kuwa zile picha kidogo tu tunazozipata katika Biblia zinatuonyesha kwamba mbinguni ni zaidi ya kukaa juu ya mawingu na kupiga vinubi.