Kuingia katika maisha ya Kikristo
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 8
SOMO 19Hatua 1 ya 8 (13%)

Kuingia katika maisha ya Kikristo

Hapa ni barua ya kusisimua sana toka kwa mmojawapo wa wawakilishi wa Shule yetu ya Biblia katika Afrika.

"Miaka mitano iliyopita nilipokea ombi toka kwa sauti ya Unabii ili nimtembelee mfungwa mmoja ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Biblia kwa Posta. Nilionyesha ombi lile kwa wakuu wa gereza lile ambao kwa hisani yao walinipa ruhusa. Kwa kuwa mwanafunzi yule alikuwa na hamu kubwa sana ya kujifunza Biblia, basi, nilimtembelea mara kwa mara.

"Karibu miezi sita baada ya kumtembelea mara ya kwanza, aliomba kubatizwa na kujiunga na kanisa. Wakuu wale walikubali kuandaa mahali ili ubatizo ule ufanyike ndani ya gereza lile. Wasimamizi wao pamoja na wafungwa wengine walikusanyika pale kushuhudia ubatizo ule niliopata kuufanya ambao uliigusa mioyo yao.

"Muda mfupi baada ya tukio lile, ndugu yetu yule alifunguliwa toka kifungoni, ingawa bado alikuwa na muda mrefu wa kutosha kutumikia kifungo chake. Nilipouliza imekuwaje, niliambiwa kwamba maisha yake yalikuwa yamebadilika kabisa, naye akawa shahidi aliyemshuhudia Mwokozi wake, na dini yake hata hakuweza tena kufikiriwa kama mfungwa wala kutendewa kama mfungwa. Mtu yule akaungana na familia yake na sasa ni kiongozi katika mojawapo ya makanisa yenye watu wengi."