Kuhusu mambo yako ya baadaye
Masomo Yote
Sehemu 1 ya 5
SOMO 07Hatua 1 ya 5 (20%)

Kuhusu mambo yako ya baadaye

Madaktari Patricia na David Mrazek walikuwa wamelemewa na huzuni kubwa sana katika kazi yao. Kama mabingwa wa magonjwa ya watoto, waliwashughulikia watoto wengi waliokuwa wakiumwa. Lakini waligundua ukweli kwamba baadhi ya watoto walitoka katika hatari yao ya kufisha na kupata nguvu mpya, ambapo wengine waliangamizwa nayo. Kwa nini? Mathalani, kwa nini mtoto mmoja atumie madawa ya kulevya wakati yule mwingine anakwenda kusoma chuoni? Kwa nini baadhi ya watoto waliotendewa vibaya wanakua na kujitendea vibaya wenyewe, wakati wengine wanakuwa wazazi wazuri?

Akina Mrazek hao walifanya utafiti wao mpana sana ili kupata majibu kwa maswali hayo. Katika uchunguzi wao tabia moja iliyozidi zote ilizidi kujitokeza miongoni mwa watoto wale walionusurika kutoka katika kiwewe chao na kuendelea kuwa na maisha "ulikuwa ni ule mtazamo wa maisha uliojengwa juu ya mwelekeo wa kutazamia kuyaona mambo mazuri siku za mbele na kuwa na matumaini."

Kuwa na tumaini kulileta tofauti ile. Tumaini, kuliko kitu kinginecho chote, linatusaidia sisi kuyashinda mambo ya ajabu-ajabu yanapokuja kwa wingi sana dhidi yetu.

Wanadamu wanalihitaji tumaini sana. Lakini, je! tunalipataje? Tumaini katika ulimwengu wetu huu ni vigumu kuliona - MPAKA tuliangalie kwa mtazamo wa unabii wa biblia. Mwongozo huu wa GUNDUA unauchunguza unabii ule wa maana sana uliowatia tumaini lenye nguvu watu wengi wasio na idadi.

1. Unabii wa Biblia Unaoshangaza

Karibu miaka mia tano hivi kabla ya kuzaliwa kwake Kristo, Mungu aliupa ulimwengu huu mtazamo wa haraka wa mambo ya mbele unaoshangaza sana kupitia kwa nabii Danieli. Mungu alitoa muhtasari wa historia ya ulimwengu huu miaka 2,500 kabla ya kutokea, kuanzia wakati ule wa Danieli mpaka siku zetu hizi.

Unabii huo ulianzia katika ndoto ambayo Mungu alimpa Nebukadreza, Mfalme wa Babeli, yapata mika 2,500 hivi iliyopita. Ndoto ile ilimsumbua sana mfalme yule - lakini hakuweza kuikumbuka ndoto ile alipoamka kutoka usingizini! Baada ya wenye hekima wote wa Babeli kushindwa kumsaidia mfalme yule kuikumbuka ndoto yake au kuifasiri, kijana mmoja Mwebrania, aliyekuwa kule uhamishoni, kwa jina Danieli, alijitokeza kwenye mandhari ile, akidai kwamba Mungu wa Mbinguni alikuwa na uwezo wa kuzifunua siri zote.

Akiwa amesimama mbele ya mfalme yule, akanena kwa ujasiri, akasema

Danieli 2:31-35
"Wewe, Ee, mfalme, ulitazama, na pale mbele yako ilisimama SANAMU KUBWA - sanamu kubwa sana, inayong'aa. "Kichwa cha sanamu ile kilitengenezwa kwa dhahabu safi, kifua na mikono yake ni ya fedha, tumbo lake na mapaja yake ni ya shaba nyekundu, miguu yake ni ya chuma, na nyayo zake nusu za chuma na nusu za udongo wa mfinyanzi uliochomwa. "Ulipokuwa ukiangalia, jiwe lilichongwa, lakini si kwa mikono ya wanadamu. Likaipiga ile sanamu katika nyayo zake za chuma na udongo na kuivunja vipande vipande. "Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba nyekundu, na ile fedha, na ile dhahabu, vikavunjwa vipande vipande wakati ule ule na kuwa kama makapi juu ya sakafu ya kupepetea wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperusha mbali bila kuacha kitu cho chote mahali pake. Lakini ULE MWAMBA ULIOIGONGA SANAMU ILEukawa mlima mkubwa, UKAIJAZA DUNIA YOTE"

Sanamu hiyo, kwa kuitupia jicho mara moja, yaweza kuonekana kana kwamba haina kazi sana kuweza kutupatia sisi tumaini katika nyakati hizi tunazoishi, lakini wewe endelea tu kusoma habari zake.

2. Unabii Watafsiriwa

Baada ya kumsimulia Nebukadreza aliyekuwa amevutiwa sana na kile alichokuwa amekiona hasa katika maono yake, nabii Danieli alitoa ufafanuzi wake:

Danieli 2:36
"Hii ndiyo ile ndoto, na sasa tutaifasiri kwa mfalme"

KICHWA CHA DHAHABU: Je, ni mamlaka gani ya dunia ambayo Danieli alimwambia yule mfalme kuwa ilionyeshwa kwa mfano wa kichwa cha dhahabu?

Daniel 2: 37,38
"Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme. Mungu wa mbinguni amekupa wewe ufalme na uwe, na nguvu, na utukufu.... WEWE U KICHWA KILE CHA DHAHABU"

Danieli alikuwa anampasha habari hizi mtawala yule wa dola kubwa kuliko zote ulimwenguni: "Nebukadreza, Mungu anakuambia wewe kwamba dola yako, Babeli,

imewakilishwa na kichwa hicho cha dhahabu cha hiyo sanamu."

KIFUA NA MIKONO YA FEDHA. Kwa mtazamo wa kibinadamu Babeli ilionekana kama dola ambayo ingeweza kudumu milele. Lakini, je, unabii unasema kitu gani kitatokea baada yake?

Daniel 2:39.
"Baada yako, utainuka ufalme ulio mdogo kuliko wako"

Kwa kutimiza utabiri huo wa Mungu, ufalme ule wa Nebukadreza ulivunjika vipande vipande na kuwa magofu wakati yule Koreshi, Jemedari wa Kiajemi,

alipoiangusha dola ile ya Babeli mwaka ule wa 539 K.K. kwa hiyo, kifua na mikono ya fedha huwakilisha Uamedi na Uajemi, dola nyingine yenye nguvu nyingi.

TUMBO NA MAPAJA YA SHABA NYEKUNDU: Sehemu hii ya sanamu ile kubwa ya madini huwakilisha nini?

Daniel 2:39
"Halafu, ufalme wa tatu, ufalme wa shaba nyekundu, utatawala juu ya ulimwengu nzima."

Tumbo na mapaja ya shaba nyekundu ni mfano wa ufalme wa Uyunani (Ugiriki). Iskanda mkuu (Alexander the Great) aliwashinda Waamedi na Waajemi, na kuingiza Uyunani kuwa dola kuu ya tatu ya ulimwengu . ilitawala kuanzia mwaka wa 331 hadi mwaka 168 K.K.

MIGUU YA CHUMA:

Daniel 2:40
"Hatimaye, patakuwa na ufalme wa nne [alisema yule nabii], wenye nguvu kama chuma - kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kukishinda kila kitu - na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta zile nyingine zote."

Baada ya kifo chake Iskanda, dola yake ilidhoofika na kugawanyika katika makundi yanayoshindana mpaka hatimaye katika mwaka ule wa 168 K.K, "Dola ya Chuma" ya Roma ikaishinda Uyunani katika vita ya Pydna.

Kaisari Augusto alitawala katika ile Dola ya Roma wakati alipozaliwa Yesu mnamo miaka elfu mbili iliyopita (Luka 2:1). Kristo na mitume wake waliishi katika kipindi kile kilichowakilishwa na miguu ya chuma. Giboni, mwanahistoria wa karne ile ya kumi na nane, bila shaka mawazoni mwake alikuwa na unabii wa Danieli, alipoandika maneno haya: "Zile sanamu za dhahabu, au fedha, au shaba, ambazo zingetumika kuyawakilisha mataifa na wafalme wao, zilivunjwa na kurithiwa na ufalme ule wa chuma wa Roma" - Edward Gibbon, The History of the Decline and Fall of the Roman Empire (John D. Morris and Company), gombo la 4, uk. 89.

Hebu kwa dakika moja tafakari juu ya utabiri huo kwa mtazamo wa kibinadamu. Je, kwa vipi Danieli, aliyeishi katika kipindi kile cha Babeli, angekuwa na wazo lo lote kuhusu dola ngapi zingefuatana moja baada ya nyingine mamia ya miaka katika siku zile za mbele. Sisi tunakuwa na wakati mgumu kukisia soko la biashara litakuwaje juma lijalo! Na, hata hivyo, Babeli, Umedi-Uajemi, Uyunani, na Roma zilifuatana kabisa moja baada ya nyingine, kama vile ilivyotabiriwa - kama watoto wa shule watiifu ambao wamesimama katika mstari.

Je, Mungu anayadhibiti mambo yale ya baadaye? Je, tunaweza kuwa na tumaini kwa kutegemea msingi wa mpango wake ule mkuu? Jibu lake ni "Ndiyo!" ivumayo kote.