Mvulana mmoja ndani kabisa ya mji anauawa kwa risasi zilizofyatuliwa ovyo na majambazi wakati anafanya kazi yake ya shuleni akiwa ameketi nyumbani kwao katika meza ya familia yake.
Mama mmoja kijana katika viunga vya mji anagundua kwamba mtoto wake amepatikana na Ukimwi kutokana na damu aliyoongezewa mwilini mwake.
Misiba inazidi kuendelea tena na tena katika ulimwengu wetu huu. Nasi tunatamani sana kujua jibu kwa mambo hayo yote. Hivi Mungu huyo yuko wapi katika ulimwengu wetu huu uliojaa mateso na vifo visivyo na maana? Mtunga Zaburi anatuhakikishia sasa kwamba " dunia hii imejaa upendo wake usio na mwisho" (Zaburi 33:5).
Lakini, basi, kama hilo ni jambo la kweli, mbona hayakomeshi mateso hayo pamoja na misiba? Sura ya 20 ya Ufunuo inatuonyesha sisi ni kwa ajili gani na lini Mungu atakapo komesha dhambi na mateso.
